UHARAMIA HUU HADI LINI?

Nafikiri sasa ifike mahali serikali ya Tanzania iwe na sheria kali kwa watu wanaofanya uharamia kama huu wa picha zinavyoonekana hapa. Chanzo kinasema hii ilitokea katika hifadhi ya wanyama ya taifa Mikumi. Inawezekana kweli waharibifu hawa wasijulikane? Uwepo ushirikiano wa karibu na wananchi wanaozunguka hifadhi zote za wanyama ili matukio kama haya yapungue lakini pia sheria kali ziwekwe. Ningewezasema sheria kali kama za China zinafaa ili kulinda mali za taifa....si wanyama tu lakini rasilimali zote za taifa. Hii binafsi imeniuma sana na natumai serikali itachukua nafasi yake mambo kama haya yasiwepo. Kingine labda serikali inatakiwa kuweka usimamizi wa rasilimali za nchi katika mitaala ya shule kuanzia msingi hadi vyuo vikuu ili kila mtu akue hivo na achukue jukumu.

Huyu Simba si kwamba anaumwa magonjwa ya kawaida ila alitegwa kwa waya na ndo inayomuua kwani iko shingoni inaendelea kumnyonga taratibu. Hatujui aliishia wapi kama kuna mwenye taarifa zaidi tujulishane, na pia kama wahusika walikamatika!!

Nafikiri kitengo kinachohusika kitaona hili.









Chanzo: http://tech.sina.com.cn/d/2012-05-23/07477150795.shtml

Post Title : UHARAMIA HUU HADI LINI?

UHARAMIA HUU HADI LINI?,

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...